11 Aug 2015

T-SUNAMI YA MAGUFULI (MWANANCHI)

Mtwara. Waziri wa Ujenzi na mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amesema kuwa wana-CCM mwaka huu wanapaswa kufanya kampeni za kisayansi zaidi kuhakikisha wanapata ushindi wa tsunami utakaowezesha kuundwa kwa Serikali imara itakayowaletea maendeleo Watanzania wote.
Alisema kwa kufanya hivyo kutawasaidia kupata viti vingi na kusimamia shughuli zote za maendeleo na kwa manufaa ya wanaCCM na Watanzania wote kwani mahitaji yao na matarajio yao ni kupata maendeleo makubwa.
“Niwaombe wana CCM wenzangu, tushikamane tuwe wamoja. Kampeni za mwaka huu ni lazima tufanye kampeni za kisayansi zaidi, ni lazima kampeni zianze katika ngazi ya nyumba kumi, vitongoji kwa vitongoji, vijiji, mitaa, kata majimbo , wilaya, mikoa na baadaye urais kwa ujumla. Katika umoja huu nataka niwahakikishie ushindi wa mwaka huu wala si wa kimbunga, ni wa tsunami,” alisema Dk Magufuli.
Dk Magufuli aliyekuwa katika ziara ya mikoa ya kusini ya kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotelekezwa katika kipindi cha awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete, alisema hayo hapo jana wakati akizungumza na wanachama wa chama hicho nje ya ofisi za CCM mkoa wa Mtwara, ikiwa ni siku moja baada ya rais kukamilisha ziara yake na kuwaaga wananchi wa mkoa huo.
Mgombea huyo na mbunge wa Chato alibainisha kuwa amekuwa kiongozi katika maeneo mbalimbali nchini kwa kipindi kirefu, hivyo anakifahamu vema chama, shida za wanaCCM na matarajio yao yanayojumuisha matarajio ya Watanzania wote na shida zao.
Alisema kuwa endapo atachaguliwa kuwa rais, hatawasahau wanaCCM na Wanamtwara kwa ujumla, lakini wote hao wanapaswa kushikamana na kuwa kitu kimoja kwa kuwa maendeleo hayana chama na akichaguliwa atakuwa rais wa Watanzania wote.
Alisema katika kipindi cha miaka 20 ya uongozi, amekuwa akifika Mtwara na hivyo ana uhakika endapo Wanamtwara wataamua kumpatia nafasi ataujua zaidi mkoa huo kuuendeleza katika kipindi cha miaka mingine zaidi.
“Wanamtwara nafahamu matarajio yenu, nataka niahidi kwenu na nimwombe Mungu nitapenda sana niwe mtumishi wa watu, nisiwe na majivuno wala kujiona, niwe mtumishi hasa wa wanyonge niweze kuwasikiliza na kusikiliza matarajio yao.
“Matarajio ya Watanzania na Wanamtwara ni makubwa, wanahitaji maendeleo makubwa na tunahitaji kuyasukuma. Nchi yetu imelelewa katika misingi ya umoja pasipo kubaguana kutokana na maeneo tunayotoka, dini, makabila hivyo tunahitaji umoja na palipo na umoja pana amani na palipo na amani pana maendeleo,” alisema Dk Magufuli.
Makundi ndani ya vyama
Akizungumzia makundi katika chama hicho, alisema  yalikuwapo zaidi ya 40 na baada ya uchaguzi makundi yote yalimuunga mkono yeye aliyepitishwa na vikao vya chama, hivyo wanaoondoka ndani ya chama hicho kwa chama kikubwa kama CCM ni jambo la kawaida kwa kuwa hata enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere wapo walioondoka na waliofukuzwa.
“Mti ambao unataka upate mbao zake nzuri, matawi kudondoka ni neema, lakini kwa watu kuondoka ndani ya CCM ni kawaida na kwa chama kikubwa kama CCM ni jambo la kawaida sana,” alisema Dk Magufuli.
Mtwara wajipanga
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara, Homamed Sinani alisema watahakikisha CCM Mtwara inaendelea kupata ushindi wa kishindo kuanzia ngazi ya udiwani, ubunge na urais.
“Chama kipo imara, mimi kama mwenyekiti wa chama mkoa nasema chama kimejipanga kikamilifu na nina imani kama mshikamano ukidumishwa tunatarajia ushindi wa vishindo kuanzia ngazi ya udiwani, ubunge hadi urais,” alisema Sinani.
JK akemea siasa chafu
Katika hatua nyingine, wakati akihitimisha ziara yake juzi, Rais Kikwete aliwataka wanasiasa mkoani Mtwara kuacha siasa chafu za kupotosha wananchi badala yake wawaambie ukweli juu ya miradi na mikakati ya maendeleo inayoendelea mkoani humo.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo juzi wakati akiweka jiwe la msingi katika tawi la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Mtwara ambalo ni la saba nchini na baadaye kuirudia wakati akihutubia mkutano wa kuwaaga wananchi.
Rais Kikwete aliwataka wananchi kutosikiliza maneno ya watu wapotoshaji wanaotafuta umaarufu wa kisiasa kwa bei nafuu.
Alisema kuwa hakuna mtu yeyote anayeweza kuzuia maendeleo ya Mtwara kwa sababu kuna fursa nyingi zinazovutia uwekezaji.
“Msisikilize maneno ya wapotoshaji wanaotafuta umaarufu wa kisiasa kwa bei nafuu, Mtwara na Lindi kulichelewa lakini kutakuwa kwa kwanza na kule kulipokuwa kumetangulia kutafuata,” alisema Rais Kikwete.
Ingawa hakufafanua, kauli hiyo ya Rais Kikwete ilikuwa inalenga vurugu za wananchi wa Mkoa wa Mtwara zilizotokea mwaka jana zikipinga usafirishaji wa gesi kwa njia ya bomba kwenda Dar es Salaam ambazo zilihusishwa na ushawishi wa kisiasa.
Hata hivyo alisema kuwa Mtwara ndio muhimili mpya wa uchumi wa Tanzania kutokana na kuwa na rasilimali nyingi zinazotoa fursa za uwekezaji hivyo kunahitajika uwepo wa huduma za kibenki kwa karibu.
“Wanasiasa wa Mtwara msiwachanganye  wananchi badala ya kuwaeleza msimamo sahihi wenye mwelekeo mnakwenda kuwapeleka kwenye mambo ambayo yanawaongezea  sifa ya muda mfupi na kuwavuruga wananchi hawa na kukosa utulivu wa kufanya mambo ya maana,”alisema Rais Kikwete.

KIPANYA ANAUTANI......


MBOWE AUGUA GHAFLA (MWNANCHI)

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe jana aliugua ghafla akiwa katika maandamano ya kumsindikiza mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, Edward Lowassa baada ya kuchukua fomu za kugombea urais katika Tume ya Taifa Uchaguzi (NEC).
Mbowe alishiriki katika maandamano yaliyoanzia Makao Makuu ya CUF yaliyopo Buguruni wilayani Ilala kuelekea NEC na baada ya Lowassa kuchukua fomu, mwenyekiti huyo aliendelea na msafara kwenda Kinondoni yalipo makao makuu ya Chadema.
Wakiwa njiani Mbowe na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu walikuwa wamechomoza kwenye gari wakiwapungia wananchi waliojitokeza kwenye maandamano hayo.
Hali ya Mbowe ilibadilika ghafla na aliamua kushuka juu ya gari na kukaa katika kiti, ndipo Lissu na watu waliokuwamo kwenye gari hilo wakaanza kumpatia huduma ya kwanza kwa kumfungua vifungo vya shati lake katika eneo la Kinondoni kwa Manyanya.
Wakati hali ya Mbowe ilipoanza kubadilika msafara wa Lowassa ulikuwa ukielekea katika Uwanja wa Biafra, Kinondoni na magari yalikuwa yakitembea mwendo mdogo kutokana na maelfu ya watu waliokuwa wakiandamana.
Wakati maandamano hayo yakiendelea, gari lililombeba Mbowe likiwa na walinzi wa Chadema walioning’inia milangoni, lilichomoka katika msafara huo ambao ulikuwa umeingia Barabara ya Kawawa na lilikunja kona katika barabara ya kuelekea Mahakama ya Kinondoni kwa ajili ya kumwahisha hospitali na taarifa zilizopatikana baadaye zilieleza kuwa lilielekea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Akizungumzia hali hiyo, Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, alisema kuwa Mbowe yuko salama na anaendelea vizuri.
“Ni uchovu, uchovu, uchovu tu but he is out of danger (hayuko katika hali ya hatari),” alisema Lissu.
Ofisa Uhusiano wa MNH, Aminiel Aligaesha alisema walimpokea Mbowe saa 11 jioni na alikuwa anaendelea na matibabu katika hospitali hiyo, hata hivyo hakutaka kuweka wazi ugonjwa uliokuwa unamsumbua

LOWASSA: WAMEISOMA NAMBA (MWANANCHI)



Dar es Salaam. Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema anayewakilisha vyama vinavyounda Ukawa, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema maelfu ya wananchi waliojitokeza kumsindikiza wakati akienda Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchukua fomu ni salamu kwa CCM na ‘wameisoma namba’ kwamba Watanzania wanataka mabadiliko.
Akiwahutubia mamia ya wafuasi wa vyama vinavyounga mkono Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) katika Ofisi za Makao Makuu ya Chadema jana, Lowassa aliyeonekana kuwa na furaha muda wote, alisema maandamano waliyoyafanya hayajawahi kutokea katika historia ya Tanzania.
“Haijatokea katika historia ya nchi yetu maandamano makubwa ya aina ile, nimefurahishwa na vijana wametembea kutoka Buguruni hadi Kinondoni na hamjachoka nawapongeza sana, asante sana,” alisema Lowassa.
Alisema ana mambo mawili ya kusema; kwanza kuwashukuru wafuasi na wapenzi wa Ukawa kwamba kwa kujitokeza kwa wingi wamepeleka meseji moja kwa wasiowatakia mema, wanaosema CUF na Chadema ni watu wenye fujo, wamethibitisha kwamba si kweli.
 “Tumewahakikishia kuwa sisi ni watu wenye nidhamu na uwezo, Mwenyezi Mungu akipenda Oktoba tunachukua nchi asubuhi peupeee, kwa hiyo watu wasitafute visingizio, watafute vingine, watoto wa mjini wanasema wameisoma namba,” alisema Lowassa huku akishangiliwa na umati wa watu.
Akizungumzia jambo la pili, mbunge huyo wa Monduli aliyejiondoa CCM siku 15 zilizopita, alisema anauchukia umaskini kiasi kwamba anauona kama ukoma.
Lowassa ambaye mara nyingi husema hajakutana barabarani na Rais Jakaya Kikwete, alisema rafiki yake huyo ndiye aliyeharibu uchumi wa nchi, lakini akasema asingetaka kutoa mashtaki bali kutoa takwimu za hali ilivyobadilika.
“Wakati Rais Benjamini Mkapa anaondoka madarakani, bei ya sukari ilikuwa Sh650, leo ni Sh2,300, kutoka 650 hadi 2,300 ameharibu uchumi, hajaharibu?” aliuliza na kujibiwa, “ameharibuuu.”
“Bei ya mchele ilikuwa Sh550 leo Sh2,200, ameharibu uchumi, hakuharibu? Sembe kilo ilikuwa Sh250 leo ni Sh1,200, ameharibu hakuharibu?” alihoji Lowassa na watu wakamjibu ‘ameharibuuu” na kisha akaongeza kuwa kwa sababu hizo, CCM haistahili kuendelea kutawala.
Lowassa alitumia fursa hiyo kuwaalika wanachama wa CCM wasioridhika na hali ilivyo kujiunga na Ukawa kwa kuwa inawezekana kutafuta mabadiliko nje ya chama hicho na kwamba wasione haya bali waangalie idadi kubwa ya vijana waliojitokeza jana.
Mgombea huyo, alisema Tanzania imeshuhudia uporaji mkubwa wa mali za Taifa, ambapo tembo wameuawa kuliko wakati mwingine wowote, hivyo kutokana na vitendo hivyo, CCM haistahili kuendelea kutawala.
Kuhusu kutunza shahada za kupigia kura, Lowassa alisema Wanaukawa hawapaswi kufanya mchezo kwa kuwa CCM imekuwapo madarakani muda mrefu watatumia kila kitu ndani ya uwezo wao kubaki madarakani.
“Na sisi tutumie kila kitu kilicho ndani ya uwezo wetu kuingia madarakani. Kitakachotuingiza madarakani ni kura, hifadhi shahada yako, shawishi na wengine, tarehe 25 Oktoba tunawatoa madarakani,” alisema.
Alisema amesikia maneno kuwa kuna mchezo wa watu wanapita mitaani wanachukua shahada za kupigia kura za wanajeshi, askari magereza wanachukua namba.
Alimuhoji mmoja wa wanasheria wa Chadema, Mabere Marando iwapo kama amesikia taarifa hizo, naye akajibu: “Kwa niaba ya wanasheria wote wa Chadema tunaahidi kitu kimoja, njama zote walizonazo kujaribu kuhujumu kura za Lowassa tutazidhibiti, njama zote walizonazo kuhujumu ushindi wa wabunge wetu tutazidhibiti, njama zote walizonazo kujaribu kudhibiti ushindi wa madiwani tutazidhibiti.”
Marando alisema mawakala wote wa vyama hivyo wanapaswa kupeleka matokeo ya vituo vyote baada ya kubandikwa saa 12 jioni na kwamba yeye hatasubiri atatangaza badala ya kusubiri saa saba usiku.
Mbatia
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia alisema maandamano yaliyofanyika jana ni historia mpya ambayo ni elimu kwa Watanzania. Ari iliyoonyeshwa tangu asubuhi inasadifu hamu ya Watanzania.
Pia, alisema Rais Kikwete ametangaza kuwa wapinzani ni maadui na kumtaka kuangalia lugha anayoitumia, kwa kuwa Ukawa watajibu kwa hoja na si matusi.
“Ninamhusia sana Rais Jakaya Kikwete amebaki na siku 75 tu za kuwa Amiri Jeshi Mkuu, ni ushauri wangu wa bure kabisa yeye na wenzake wachunge sana ndimi zao, maslahi ya taifa kwanza vyama baadaye, tunampa nishani iwapo atamaliza siku 75 kwa amani na kumkabidhi Amri Jeshi Mkuu, Edward Lowassa,” alisema Mbatia. “Rafiki yangu (Ibrahimu)Lipumba amekimbia akidhani Ukawa utaparaganyika lakini sasa umeimarika zaidi,” alisema Mbatia huku akishangaliwa na umati wa watu na kumaliza kuwa “Hakuna mwanadamu ambaye yupo juu kuliko wengine au taasisi yoyote.”
Makaidi
Mwenyekiti wa NLD Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, Dk Emmanuel Makaidi alisema kuwa katika umri wake mkubwa alionao hajawahi kuona maandamano ya watu wengi kama waliojitokeza kumsindikiza Lowassa jana.
“Nina miaka 74 lakini sijaona kitu kama cha leo nakaanza kujiuliza hii maana yake nini? Nikachukua mfano kama mimi ni chama tawala na wapinzani ni wengi namna hii ningeanza kufanya nini, ningejiuzulu mara moja,” alisema Makaidi.
Kaimu Mwenyekiti wa CUF, Twaha Tasilima alisema kuwa walioleta siasa mbaya nchini wanatakiwa kuwajibika kwa kuwa wamesababisha kuwapo kwa uchumi mbaya pia.
“Lowassa akiingia Ikulu ataenda kuondoa uchumi na siasa mbaya,” alisema Tasilima.
Maalimu Seif
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad alisema umati mkubwa wa vijana waliojitokeza kumsindikiza Lowassa umedhihirisha kuwa watu walikuwa wamekata tamaa sasa wanataka matumaini mapya.
Hata hivyo, alisema haitoshi kumsindikiza Lowassa kwa idadi kubwa namna hiyo kama hawataenda kupiga kura kwa kuwa maandamano hayawezi kuiondoa CCM madarakani.
“Hatutaishinda CCM kwa maandamano bali kwa kupiga kura, tunza kadi yako zimebaki siku chache,” alisema Hamad.
Onesmo Ole Nangolo
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole, alipokewa rasmi na kusema alijiunga CCM mwaka 1977, lakini alichokishuhudia Dodoma kwenye uchaguzi wa mgombea wa Rais kwa tiketi ya chama hicho kimemlazimisha kuhamia Chadema.
“Ile CCM niliyokuwa naifahamu si tuliyokwenda juzi Dodoma, misingi na haki imegeuka, kimekuwa chama cha viongozi wachache kwa maslahi yao binafsi, unyanyasaji umetawala ndani ya CCM, sina moyo wa chuma,  sikuridhika na mchakato wa Dodoma,” alisema Nangolo.
Ilivyokuwa
Jiji la Dar es Salaam lilisimama kwa wastani wa saa nane kutokana na msafara wa Lowassa kwenda kuchukua fomu.
Makundi ya watu wa kada mbalimbali wakiwamo madereva wa bodaboda, bajaji, magari na watembea kwa miguu walionekana kufunga barabara ya Uhuru kuanzia Buguruni eneo la Rozana zilipo ofisi za CUF na Posta zilipo ofisi za NEC.
Maandamano hayo yalisababisha msongamano wa magari na kusababisha magari ya abiria maarufu kama daladala na magari binafsi kutafuta njia mbadala kufanikisha safari zao.
Idadi ya watu waliojitokeza katika msafara inaweza kufananishwa na ile iliyojitokeza wakati wa ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama Julai 2013.
Watu wengi walionekana wakitumia simu kupiga picha na kurekodi video za matukio mbalimbali pembeni mwa barabara huku wengine wakiwa juu ya maghorofa wakitazama.
Wapo waliokuwa wakitoka maofisini na kukaa pembezoni mwa barabara kushuhudia tukio hilo huku maelfu wakitembea umbali wa kilometa sita kuufuata msafara huo.
Msafara huo ulitumia saa mbili na nusu kutoka Buguruni hadi ofisi za NEC.
Kabla ya msafara
Wafuasi wa vyama vinavyounda Ukawa; CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi na NLD walianza kukusanyika tangu saa moja asubuhi katika makao makuu ya CUF yaliyopo Buguruni na viongozi mbalimbali walianza kuingia saa 3:56 asubuhi na kumkuta mwenyeji wao Maalimu Seif.
Wengine
Makundi ya mashabiki waliokuwa wakizunguka wakiimba nyimbo mbalimbali, ukiwamo; ‘kama siyo juhudi zako Kikwete, Lowassa tungempata wapi? Na wengine wakikejeli, “Magufuli toroka uje, Tanzania mpya bila CCM inawezekana, tumechoka kuokota makopo na funguo za Magufuli zipo Ukawa.
Safari ya Biafra
Baada ya kukabidhiwa fomu na Ofisa Mwandamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Deogratius Nsanzugwanko, Lowassa, mgombea mwenza, Juma Duni Haji na viongozi waandamizi wa Ukawa waliendeleza msafara wa kwenda Makao Makuu ya Chadema mtaa wa Ufipa, Kinondoni.
Licha ya umati uliomsindikiza kutembea kilomita nane ukitoka Buguruni, idadi ya watu ilizidi kuongezeka na kuendeleza maandamano yaliyoanzia makutano ya mtaa wa Ghana na Ohio ilipo NEC kupitia Barabara ya Barack Obama na kuunga hadi Ali Hassan Mwinyi.
Kama ilivyokuwa awali, wafuasi hao waliendelea kuimba bila kuchoka nyimbo mbalimbali za hamasa ili wasichoke na kila eneo walilokuwa wakipita umati mkubwa wa watu waliojipanga katika barabara hizo ulishangilia na hata kuwafanya baadhi ya waliokuwamo kwenye magari kuonyesha alama ya “V” inayoyotumika na Chadema.
Msafara ulizidi kuongezeka urefu baada ya wale waliochelewa kuungana nao na baadaye uliiacha barabara ya Ali Hassan Mwinyi na kuingia barabara ya Kinondoni ambayo kutokana na wembamba wake iliwalazimu wenye magari waliokuwa safarini kuegesha pembeni kupisha watu waliokuwa wakiandamana.
Katika safari yote hiyo, polisi walikuwa wameegesha magari yao katika kila umbali wa kilomita moja na nusu au zaidi na kufanya umati huo uwashangilie kila unapowapita.
Licha ya kuwa taarifa za awali zilibainisha kuwa maandamano hayo yangeishia Makao Makuu ya Chadema, ilibidi uongozi wa chama hicho ubadilishe utaratibu na kuwapeleka watu wote katika Viwanja vya Biafra, Kinondoni kwa kuwa eneo la mtaa wa Ufipa lisingetosha.
Walipofika Biafra baada ya kumaliza takribani kilomita saba kutoka NEC, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu aliwasalimia wafuasi hao na kumkaribisha Lowassa awashukuru ambaye alizungumza kwa ufupi akitamka maneno, “hii haijawahi kutokea.”
Lowassa aliwapongeza polisi kwa kufanya kazi kwa weledi na kueleza kuwa busara na amani vilivyotumika katika maandamano hayo vinadhihirisha kuwa Chadema na Ukawa ni vyama vya kushika dola.
Baada ya watu kutawanyika, msafara wa viongozi ulirudi mtaa wa Ufipa kuendeleza hotuba ambako baadhi ya wafuasi walioshtukia kuwa walidanganywa walirudi kwenda kuwasilikiliza viongozi.

11 Apr 2015

UCHAMBUZI HUU JUU YA ZITO

http://fullhabari.blogspot.com/2015/04/mauchafu-ya-zitto-kabwe-haya-hapaageuza.html?m=1

KUTOKA MAGAZETINI

http://www.mwananchi.co.tz/Makala/Choki--Kuendesha-bendi-ni-pasua-kichwa/-/1597592/2682518/-/p9w834/-/index.html

21 Mar 2015

19 Mar 2015

MTUMISHI WA BWANA AKUTWA NA VIUNGO....

Check out @millardayo's Tweet: https://twitter.com/millardayo/status/578614129071669248?s=09

17 Mar 2015

Republican congressman resign

http://news.yahoo.com/congressman-aaron-schock-to-resign--report-183223696.html Rep. Aaron Schock said in a written statement that he will resign from his seat in Congress effective March 31. The Illinois Republican's spending of campaign and taxpayer money have come under heavy scrutiny in the past six weeks.

16 Mar 2015

ZITO AIBUA MAPYA

Check out @millardayo's Tweet: https://twitter.com/millardayo/status/577699424794722304?s=09

15 Mar 2015

FERGUSON

http://news.yahoo.com/police-announce-arrest-ferguson-police-shootings-175442302.html CLAYTON, Mo. (AP) — Authorities said Sunday they've made an arrest in the shooting of two officers outside the Ferguson Police Department.

TAARIFA TOKA TFF

https://www.scribd.com/mobile/doc/258776137/embed?access_key=key-EbjY2laSTIokUXsQJJYt

MWANAKIJIJI

NIDHAMU

Check out @MwananchiNews's Tweet: https://twitter.com/MwananchiNews/status/577046750332092416?s=09

Umeelewa nn

Mhh...

Check out @citizentvkenya's Tweet: https://twitter.com/citizentvkenya/status/576818489115168768?s=09

LOWSSA:KINANA NI JEMBE

Check out @millardayo's Tweet: https://twitter.com/millardayo/status/576996982482419712?s=09

MAFURIKO

Check out @UN's Tweet: https://twitter.com/UN/status/577024091439394816?s=09

UGAIDI PAKISTAN

Check out @BBCBreaking's Tweet: https://twitter.com/BBCBreaking/status/577024770002317312?s=09

14 Mar 2015

HISTORIA YA MC PILI PILI

Check out @bongofive's Tweet: https://twitter.com/bongofive/status/576701151053238272?s=09

Pitia hiyo

Check out @WorldBank's Tweet: https://twitter.com/WorldBank/status/576639136804827136?s=09

Pitia hapo

Check out @GhaflaKenya's Tweet: https://twitter.com/GhaflaKenya/status/575683670607986688?s=09

11 Mar 2015

MTOTO WA AJABU AZALIWA SHINYANGA

 

Afariki
. Baada ya dakika 20
Taarifa ambayo kwanza ilianza kuenea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ajali ya basi la abiria na lori la mizigo,kwamujibu wa mashuhuda kutoka eneo la Changarawe, Iringa ambapo wamesema ni kweli ajali hiyo imetokea na kuna idadi kubwa ya watu ambao wamefariki.
Mashuhuda wamesema basi la Majinja lilitokea Mbeya kuja Dar es Salaam limegongana na lori la mizigo katika eneo hilo, abiria waliofariki ni wengi japo idadi kamili haijafahamika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, kwa sasa yuko njiani kuelekea eneo la tukio ili kuona mazingi
ra ya ajali na kutoa taarifa kamili kuhusu ajali hiyo zitakujia kadri tutakavyo kuwa tukipokea.

10 Mar 2015

KOCHA YANGA ACHOSHWA NA VIPIGO SIMBA

KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans Van Der Pluijm, amesema kama ataendelea kukinoa kikosi hicho, anaamini atafuta uteja wa kufungwa na watani wao wa jadi, Simba, ambao mara yao ya mwisho kuwafunga katika ligi ilikuwa msimu wa 2012/ 2013.
Yanga, ikiwa inanolewa na kocha Mholanzi, Ernest Brandts, iliibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Simba Mei 19, 2013, huku Wanajangwani hao wakiweza kuibuka mabingwa wa msimu huo.
Akizungumza na MTANZANIA jana, baada ya kufungwa bao 1-0 na wekundu hao wa msimbazi, Pluijim alisema matokeo ya kushindwa kufanya vizuri kila wanapokutana na Simba yanakaribia kumalizika, kwani mara kadhaa wanapokutana mbali na mechi za ligi wamekuwa wakifungwa.
“Tutamaliza hili suala la kufungwa, kila kitu kinahitaji muda, hii ni mara yangu ya pili kukiongoza kikosi changu kuvaana na Simba, katika mchezo wetu wa mzunguko wa pili, msimu wa 2013/2014 tulitoka sare bila kufungana,” alisema Pluijm.
Alisema wakati anakabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo kutoka kwa Brandts, ambaye alitimuliwa na uongozi kutokana na matokeo mabovu, aliweza kuwadhibiti Simba.
Mbali na kauli yake hiyo, Pluijm alimzungumzia mchezaji Emmanuel Okwi kuwa ni mchezaji hatari na wa kuogopwa.
“Okwi ni mchezaji hatari, kwani anaweza kubadilisha matokeo wakati wowote, ogopa mchezaji kama huyo,” alisema.
Alieleza katika mchezo wa juzi aliamua kumtoa Danny Mrwanda, ili kuepusha ugomvi, kwani tayari mchezaji huyo alionyesha kuwa tatizo uwanjani.
“Nilimtoa Mrwanda nikiwa na maana yangu, hakuwa vizuri kabisa, nililiona hilo, nilichokifanya ni kumwepushia kadi nyekundu, alionekana kuwa na jazba,” alisema Pluijm.
Mholanzi huyo alikwenda mbali zaidi na kusema tukio la mchezaji wake, Haruna Niyonzima kupewa kadi nyekundu limemuumiza sana na litamlazimu kufanya mazungumzo ya kina kufahamu ukweli kutoka kwa kiungo huyo.
Wakati huo huo, Niyonzima alipozungumza na gazeti hili, aliwatupia lawama mashabiki na kudai wao ndio waliosababisha apewe kadi kutokana na makelele yaliyopelekea ashindwe kusikia mlio wa filimbi.
“Sina kosa lolote mimi, unajua zile kelele za mashabiki bwana kila mtu anaongea lake, wakati ule unakuta na sisi wachezaji vichwa vinawaza mabao,” alisema Niyonzima.
Upande wa nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, alisema hakuna haja ya mabeki wao kulaumiwa, kwani walionyesha kiwango kizuri, ila bao alilofunga Emmanuel Okwi lilikuwa bora zaidi.

FLORA MBASHA: NIKOTAYARI KURUDI KWA EMMANUEL


MUIMBAJI wa muziki wa Injili, Flora Mbasha amesema yupo tayari kurudiana na mume wake Emmanuel Mbasha, ikiwa atakwenda kumuangukia miguuni na kumuomba msamaha.
Flora alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake juu ya kesi ya ubakaji inayomkabili Mbasha ambayo inasikilizwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala.
“Mbasha nimemsamehe siku nyingi na nipo tayari kuishi naye iwapo atakuja kuniangukia miguuni na kuniomba msamaha… lakini hili (ubakaji) ni suala la mahakama,” alisema.
Alipoulizwa baba halali wa mtoto wake wa kike aliyejifungua hivi karibuni, alisema hawezi kulizungumzia jambo hilo hivi sasa.
“Siwezi kulizungumzia nikifanya hivyo nitakuwa simtendei haki mwanangu. Siwezi kubadili mitizamo ya watu jinsi wanavyotafakari kuhusu jambo hili,” alisema.
Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga alisema awali Flora alitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Flora Mjaya na kueleza alivyosimuliwa na binti huyo anayedai kubakwa na Mbasha.
Katuga alikuwa akitoa ufafanuzi huo kwa waandishi kwa vile kesi hiyo inasikilizwa katika mahakamani ya siri kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa makosa ya jinai ya mwaka 2003 sura ya 20 kifungu cha 186, kifungu kidogo cha tatu ili kulinda haki ya binti huyo.
Wakili alisema Flora aliieleza Mahakama kuwa Mei 23 mwaka jana, alimkuta binti huyo akiwa mnyonge huku amelala kitandani na kujifunika shuka.
Alisema alimhoji binti huyo kama alikuwa anaumwa au la lakini hakumjibu chochote.
Flora alisema siku iliyofuata Mei 24, waliondoka na kwenda kanisani yeye na watoto waliokuwapo nyumbani lakini Mbasha hakuongozana nao.
“Flora alipotoka kanisani na watoto aliwarudisha nyumbani kisha akaondoka na kwenda hotelini kwa sababu alikuwa na ‘stress’ (mawazo) lakini akiwa huko alipigiwa simu na mdogo wake Suzan (shahidi wa pili) akimueleza kile alichoambiwa na binti huyo,” alisema Katuga.
Alisema Flora baada ya kuambiwa jambo hilo kwa simu alimwambia mdogo wake huyo ampeleke binti huyo katika hoteli iliyoko Sinza.
Alisema walipofika binti huyo alimsimulia tukio hilo la kubakwa na ndipo akawaambia waende wakatoe taarifa hizo kituo cha polisi kabla ya kwenda hospitalini.
Mahakama hiyo ilisikiliza ushahidi wa Flora kwa takriban saa nne.
Awali wapiga picha walizuiliwa na ndugu zake kumpiga picha huku wakidai kuwa watawashtaki.
“Mnataka kumpiga picha za nini, mmetumwa… mnajua sheria za nchi nyinyi,” alisikika mmoja wa ndugu zake.
Tukio hilo lilizua minong’ono mingi kutoka kwa wananchi waliofika mahakamani hapo kufuatilia kesi mbalimbali.
“Jamani kwani hawa si wapiga picha… waandishi si wanaruhusiwa kuchukua matukio na kwenda kuyaripoti kulikoni hawa wazuiliwe…jambo hili linashangaza kweli kweli,” alisema mwanamke mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
Tukio hilo lilimshangaza pia Wakili George Mwalali aliyekuwa mahakamani hapo ambaye alisema kitendo hicho ni kosa.
“Haiwezekani mzuiliwe kupiga picha mpo sahihi kwa sababu hapa ni nje ya Mahakama, nitakwenda kuzungumza na wakili mwenzangu juu ya jambo hili,” alisema.
Baadaye ndugu hao wa Flora waliwafuata waandishi na kuwauliza kwa nini walikuwa wakipiga picha hizo na kudai kuwa walikuwa wakiwazuia kwa vile walipata taarifa kwamba kuna mtu amewapa fedha wapige picha hizo.
“Hapana ndugu yangu, sisi hakuna aliyetupatia fedha… tunachotaka ni habari hii na si vinginevyo,” alisema mmoja wa wapiga picha.
Mmoja wa ndugu hao alisema kilichokuwa kikiwaogopesha na kuamua kuzuia utekelezaji wa hatua hiyo ni kitendo cha baadhi ya waandishi kuweka kwenye mitandao ya jamii habari ambazo si sahihi.
“Kwa mfano zile picha zilizosambazwa mwanzoni zilitushangaza kwani si za huyu binti aliyebakwa, sijui walizitoa wapi, huko ni kuchafuliana majina,” alisema.
Baada ya ndugu hao kuridhishwa na ufafanuzi waliopewa na wapiga picha waliokuwa mahakamani hapo waliwaruhusu kuendelea na kazi yao.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi April 16 mwaka huu itakapotajwa tena.

MALOPE KUTUMBUIZA PASAKA

RAIA wa Afrika Kusini ambaye ni mwanamuziki wa injili, Rebecca Malope, amethibitisha kuwa mmoja wa waimbaji wa kimataifa watakaotumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka litakalofanyika nchini.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama, sambamba na Malope, Afrika Kusini wanatarajia kutoka waimbaji wengine wawili ambao ni Solly Mahlangu na Sipho Makabane.
Msama alisema waimbaji wengine waliokubali kutumbuiza kwenye tamasha hilo ni pamoja na Ephraim Sekeleti, Solomon Mukubwa, Upendo Nkone na Bonny Mwaitege,
Naye mjumbe wa kamati ya maandalizi, Khamis Pembe, alisema wako katika mipango mikubwa ya kufanikisha miaka 15 ya tamasha hilo ambalo litaongeza ukaribu na jamii yenye uhitaji maalumu.

HATIMAYE ZITO OUT CHADEMA


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemvua rasmi uanachama Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
Hatua hiyo ya Chadema imekuja baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutupa kesi iliyofunguliwa na Zitto dhidi ya Bodi ya Udhamini ya chama hicho na Katibu wake, Dk. Willibrod Slaa.
Kesi hiyo ilitupwa jana na Jaji Richard Mziray baada ya kupitia hoja za mapingamizi matano yaliyowasilishwa na mawakili wa Chadema.
Baada ya kutolewa kwa uamuzi huo wa mahakama, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, alizungumza na waandishi wa habari na kusema tangu Zitto alipokishtaki chama hicho mahakamani, kwa mujibu wa kanuni na maadili ya viongozi wa chama hicho, alishajifukuzisha uanachama.
“Kwa mujibu wa kanuni zinazohusu maadili ya viongozi ya chama chetu, kanuni ya 10 inaeleza kuwa pale mwanachama anapokishtaki chama mahakamani anakuwa amejifukuzisha uanachama,” alisema Lissu.
Kutokana na hali hiyo, Lissu alisema tangu walipowachukulia hatua aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na Mjumbe wa Kamati Kuu, Profesa Kitila Mkumbo, walishamalizana na Zitto bali kilichokuwa kimebaki ni kusubiri uamuzi wa mahakama.
Alisema kwa mujibu wa Katiba ya chama chao, Kanuni ya Maadili ya Wabunge na Madiwani, Zitto si mwanachama wa Chadema na wala si mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Lissu alisema kwa sasa wanafuata utaratibu wa kumwandikia barua Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) ili kumtaarifu kwamba Zitto si mwanachama wa chama hicho.
“Kilichobaki sasa tutamwandikia barua mwenyekiti wa NEC kutimiza tu taratibu kwamba huyu Zitto si mwanachama wa Chadema na kama tulikuwa tuna madeni tumeshalipana.
“Sasa baada ya sisi kumwandikia barua mwenyekiti wa NEC, na yeye atamwandikia Spika wa Bunge ili amwandikie tena Zitto kuwa si mbunge wala mwanachama wa Chadema.
“Itakumbukwa kuwa tangu tulipowachukulia hatua Mwigamba, Kitila na Zitto, chama chetu kilitabiriwa mauti, sasa badala ya mauti chama kimepata nguvu sana na ile migogoro ya chini kwa chini na majungu tuliyamaliza, kwa sasa tuna nguvu kubwa kuliko wakati wowote ule,” alisema Lissu.
Alipoulizwa endapo Kamati Kuu itakaa kwa siku za karibuni kujadili suala hilo, alisema hawawezi kuitisha kikao chochote kuhusu Zitto kwa sababu walishamaliza na hawana mjadala tena.
“Naomba ieleweke kwamba ule udharura wa wakati ule mara Kamati Kuu inakaa kwa ajili ya masuala ya Zitto haipo tena, kwa sababu ile mipango ya maasi tulishakamata na Kamati Kuu haiwezi kuitisha kikao cha dharura labda kuja kusherehekea ushindi.
“Katiba yetu iko wazi na kwamba ‘consequence’ (matokeo) ya kwenda mahakamani ndiyo hayo. Sasa ni kwamba aliyetushinda akaenda mahakamani sasa tumemshinda… huyu si mwanachama wetu tena na Kamati Kuu haiwezi kujadili kwa sababu kwa kwenda tu mahakamani si mwanachama ,” alisema.
Lissu alisema Kamati Kuu itakapokaa kujadili mambo mbalimbali ya chama, itatambua rasmi kuwa Zitto si mwanachama wa Chadema.
Alisema wale ambao walikuwa wakimdanganya Zitto kwa nia ya kuiharibu Chadema, sasa watafute kitu kingine.
Lissu alisema Zitto tangu akiwa naibu katibu mkuu wa Chadema, alikuwa akifahamu Katiba ya chama hicho ya mwaka 2006 ya makatazo hayo ya mwanachama kukimbilia mahakamani.
Alipoulizwa mahusiano ya Zitto na Chadema tangu alipokimbilia mahakamani yakoje, Lissu alisema chama chao hakijawahi kuwa na mahusiano yoyote tangu alipokwenda mahakamani.
Alisema kwa sasa jopo la mawakili wa chama hicho lililokuwa linashughulikia kesi hiyo, litakaa na kuandaa gharama zote za usumbufu ili waweze kulipwa na Zitto.
Hata hivyo, alipoulizwa ushirikiano ambao ulionekana kumaliza tofauti zao kati ya Chadema na Zitto, hasa katika sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow, Lissu alisema wabunge wa chama hicho walikuwa wakiunga mkono taarifa ya Kamati ya PAC na si Zitto.
“Pale tulipomfuta nafasi ya unaibu katibu mkuu wa chama tulizungumza na Watanzania na tulifika Kigoma Kaskazini tukawaeleza wananchi kwamba kiongozi waliyemchagua amekisaliti chama na kwamba chama hakiwezi kuwavumilia kina Yuda Eskarioti, na kwamba atapata malipizi ya usaliti,” alisema Lissu.
Itakumbukwa kuwa Kamati Kuu ya Chadema iliwavua nyadhifa zao Mwigamba na Profesa Kitila kwa kuandaa waraka wa mkakati wa mabadiliko ambao ulilenga kukiangamiza chama hicho.
Katika waraka huo, Zitto anatambulika kama MM (Mhusika Mkuu), Profesa Kitila M1(Mhusika wa Kwanza) na Mwigamba M3 ( Mhusika wa Tatu).
KESI YA ZITTO
Kesi ya Zitto ilivuta hisia za watu wengi na kuwafanya wanachama wa Chadema kugawanyika makundi mawili ambapo kila ilipokuwa ikitajwa walikuwa wakijazana mahakamani.
Zitto aliomba zuio la muda asivuliwe uanachama wake na Chadema ambapo mahakama ilikubali, lakini kutokana na mgawanyiko wa wanachama, alipata wakati mgumu kwani walikuwapo waliokuwa wakimzomea na wengine walitaka kumpiga.
Wakati wote wa kesi, polisi walikuwa na wakati mgumu kumnusuru Zitto hali iliyowalazimu kutumia nguvu nyingi kutuliza ghasia na ngumi zilizokuwa zikitokea nje ya mahakama.
Mawakili wanaoiwakilisha Chadema na Bodi ya Wadhamini ya chama hicho, Peter Kibatala, Lissu na John Mallya waliwasilisha hoja kumpinga Zitto.
Katika mapingamizi hayo, walidai kesi hiyo kufunguliwa Mahakama Kuu haikuwa sahihi kwa kuwa ilipaswa kufunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ama Mahakama ya Hakimu Mkazi kwa mujibu wa sheria na muundo wa kesi za madai.
Pia kesi ilikosewa kufunguliwa katika Masijala Kuu ya Mahakama Kuu baada ya kusajiliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Jaji Mziray alisema baada ya kupitia hoja hizo na zilizojibiwa na wadai, mahakama imeamua kukubaliana na hoja za mapingamizi yaliyowasilishwa na imeamua kutupilia mbali kesi hiyo na imeamuru Zitto kuilipa gharama za kesi Chadema.
Zitto alifungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Januari mwaka jana, ikapangwa kusikilizwa kwa Jaji John Utamwa na baadaye kuhamishiwa kwa Jaji Mziray.
Katika kesi ya msingi, Zitto aliiomba mahakama iiamuru Kamati Kuu ya chama hicho na chombo chochote cha chama hicho kutojadili na kuchukua uamuzi kuhusu uanachama wake hadi rufani yake itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi na Baraza Kuu la chama hicho.
ZITTO: NAPIGA KAZI
Tulimpotafuta Zitto ili kupata maoni yake baada ya uamuzi wa mahakama kutupa shauri lake na Chadema kumfukuza uanachama, alisema kwa sasa anaendelea na majukumu yake ya kazi na hana taarifa kuhusu suala hilo.
“Kwa sasa tumetulia, ninaendelea na shughuli zangu kama kawaida… nipo napiga mzigo, ila ninashauriana na mwanasheria wangu cha kufanya baada ya kupata taarifa rasmi ndiyo tutaeleza nini cha kufanya,” alisema Zitto.
MWANASHERI WA ZITTO
Kwa upande wake, mwanasheria wa Zitto, Albert Msando, alisema hana taarifa rasmi ya hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu kuhusu mteja wake na kufukuzwa uanachama wa Chadema.
Katika taarifa yake kwa umma kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, Msando alidai taarifa ya uamuzi wa Mahakama Kuu alizipata kupitia mitandao ya kijamii hali ya kuwa kesi yao ilikuwa imepangwa kusikilizwa Machi 12, mwaka huu.
“Kesi awali ilikuwa imepangwa Machi 12 (kesho), lakini kwenye rekodi inaonekana ilirudishwa nyuma na maamuzi hayo kusomwa leo (jana) bila sisi kuwa na taarifa.
“Tunafanya utaratibu wa kupata nakala ya maamuzi ili kujua nini cha kufanya, hatuna taarifa rasmi za kufukuzwa Mheshimiwa Zitto uanachama,” alisema Msando.
Alisema taratibu zote zitafuata endapo watapokea taarifa rasmi kutoka mahakamani na ndani ya chama, na kusisitiza kuwa ana matumaini jambo hilo halitoleta chuki zisizokuwa na sababu kati ya wahusika.
KUELEKEA ACT
Taarifa za ndani zinaeleza Machi 14, mwaka huu, Zitto atafanya mkutano mkoani Kigoma kwa lengo la kuwaaga wapigakura wake ambapo atatangaza rasmi kujiunga na chama kipya cha siasa cha ACT-Tanzania.
Mbali na hilo, Machi 18, mwaka huu alikuwa na mpango wa kutumia Bunge kuwaaga wabunge na kutangaza safari yake mpya ya mwelekeo wa kisiasa akiwa nje ya Chadema.
SAFARI YA ZITTO CHADEMA
Zitto alishika nafasi kadhaa za uongozi Chadema kabla ‘hajakorofishana’ na viongozi wenzake. Kwanza, alikuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje mwaka 2004 na wakati huo huo akiwa pia Mkurugenzi wa Uchaguzi na Kampeni.
Mara baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge mwaka 2005, alichaguliwa kuwa Katibu wa Wabunge wa Chadema.
Mwaka 2007 alichaguliwa na Baraza Kuu la Chadema kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara, nafasi ambayo aliishikilia hadi mwaka jana baada ya kuondolewa na Kamati Kuu ya chama hicho.
Ndani ya Bunge, Zitto alipata kuwa Mwenyekiti wa iliyokuwa Kamati ya Mashirika ya Umma (POAC) na baadaye kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ambayo anaitumikia hadi sasa.

9 Mar 2015

MJUE EDWARD LOWASSA

Edward Lowassa,
Is a Former Prime Minister of The United Republic of Tanzania and the incumbent Member of Parliament for Monduli Constituency in Arusha Region, Northern Tanzania. He represents the ruling party, Chama cha Mapinduzi (CCM). Honourable Lowassa was born on August 26th, 1953 in Monduli. He was raised up in the Ngarash area of Monduli Township and is the eldest son of The Late Mzee Ngoyai Lowassa.

Member of Parliament
Monduli Constituency - Arusha, Tanzania
October 1990 – Present (23 years)

Prime Minister
Tanzania
2005 – 2008 (3 years)

As Minister of Water and Livestock Development
The Government of Tanzania
2000 – 2005 (5 years)Tanzania

Minister of Lands, Housing and Urban Development
The Government of Tanzania
1993 – 1995 (2 years)Tanzania

Minister of State, Prime Minister and First Vice President’s office (Policy Coordination)
The Government of Tanzania
1990 – 1993 (3 years)Tanzania

Edward Lowassa
/ Edward Lowassa

RAIA 500 WAIZUNGUKA NYUMBA MOSHI

ZAIDI ya raia 500 wameizingira nyumba moja iliyokuwa imewafungia ndani watoto 18 wenye umri kati ya miaka mitatu na 17 mjini Moshi.
Watoto hao inadaiwa walifungiwa kwenye nyumba hiyo yenye vyumba vinne na choo kimoja ambapo inadaiwa walikuwa wakifundishwa masomo ya dini.
Inaelezwa kuwa watoto hao walifungiwa kwenye nyumba hiyo kwa muda wa miaka mitatu, huku wakifundishwa masomo ya dini hali iliyozua hofu kwa wakazi wa Manispaa ya Moshi.
Taarifa za kuwapo kwa watoto hao zilibainika juzi jioni mjini hapa hali iliyovuta hisia za wakazi hao, huku wengi wao wakitaka kujua lengo la watoto hao kuwa eneo hilo na hali zao kiafya.
Hali hiyo ililazimu Jeshi la Polisi kuingilia kati na kuimarisha ulinzi ambapo waliwatoa watoto hao, huku wakitawanya wananchi hao waliokuwa wameizingira nyumba hiyo.
Chanzo cha kuaminika kutoka mjini hapa kiliiambia MTANZANIA kuwa watoto hao waliokusanywa katika nyumba hiyo wanatoka katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Mwanza.
Akizungumza na wananchi waliokuwapo eneo hilo, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga, alisema walipata taarifa ya kuwapo kwa watoto hao kutoka kwa msamaria mwema.
Alisema taarifa hiyo waliipata juma lililopita na kuanza kufanya uchunguzi wao na juzi ndipo walipokamilisha na kufika kwenye eneo hilo.
Polisi walizingira nyumba hiyo kuanzia saa 12:00 jioni hadi jana baada ya kutolewa kwa watoto hao.
Mkuu huyo wa wilaya, alisema kitendo cha kuwakusanya watoto sehemu moja bila kibali ni kinyume cha sheria.
Alisema mmiliki wa nyumba hiyo alipaswa kuomba kibali kwa mamlaka husika kwa mujibu wa sheria na si kufanya suala hilo kienyeji.
“Mafunzo anayoyatoa kwa watoto hawa, hata kama ni ya dini, ni lazima yafuate taratibu za nchi. Sheria zipo, unapokusanya watoto mahala pamoja kunatakiwa kuwaje kuanzia mazingira hadi eneo lenyewe na kama una taasisi unaendesha mafunzo, je kituo kimesajiliwa? Na ndiyo maana tumeagiza watoto warudishwe kwa wazazi wao,” alisema Makunga.
Nyumba hiyo yenye idadi ya vyumba vinne na choo kimoja, imewafanya viongozi mbalimbali walipofika eneo hilo kupata wasiwasi kutokana na idadi kubwa ya watu wanaoishi humo.
Kwa upande wake, mmiliki wa nyumba hiyo, Abdulnasir Abdulrahman, alisema wamewakusanya watoto hao ili kuwafundisha masomo ya dini ya Kiislamu na kuwakuza katika imani hiyo wakiwa wadogo.
Alisema watoto hao wameletwa hapo kwa ajili ya kupata elimu ya dini, na wazazi wao wanajua na wanachangia vitu mbalimbali ikiwamo vyakula ili kuhakikisha watoto wao wanapata elimu
ya dini ya Kiislamu.
“Watoto wote tunaoshi nao hapa wana wazazi wao, ambao wamekubaliana na sisi waendelee kupata elimu hiyo hapa chini ya uangalizi wetu na wazazi wao wamekubaliana kuwalea,” alisema Abdulrahman.
Jeshi la Polisi linawashikilia baadhi ya wazazi na mmiliki wa nyumba hiyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

PARACETAMOL HUFUPISHA MAISHA YA BINADAMMU


MATUMIZI ya kila siku ya dawa za kupunguza maumivu za paracetamol huongeza hatari ya ugonjwa wa moyo, kiharusi na kufupisha maisha ya binadamu, utafiti mpya umeonya.
Paracetamol hupendelewa zaidi na madaktari wengi hudai zi salama kulinganisha na aspirin, ambayo imehusishwa na kuvuja damu tumboni na ibuprofen iliyohusishwa na magonjwa ya moyo na kiharusi.
Lakini watafiti wa Uingereza waliofanya uchunguzi huo uliowahusisha wagonjwa 666,000 wanasema hatari iliyomo katika dawa hizo huenda ilipuuzwa na sasa wameagiza uchunguzi ufanywe kuhusu usalama wake.
Taarifa hizo iwapo ni za uhakika, itakuwa pigo kwa wengi kwa vile paracetamol zimezoeleka kuliko dawa nyingine yoyote ile ya kupunguza maumivu, na inapatikana kirahisi na kila mahali.
Nchini Uingereza kwa mfano, ushauri zaidi ya milioni 22.5 kutoka kwa daktari wa kutumia dawa hutolewa kila mwaka.
Zaidi ya hayo, makasha milioni 200 ya paracetamol huuzwa kila mwaka.
Hata hivyo, Profesa Philip Conaghan wa Taasisi ya Dawa ya Rheumatic and Musculoskeletal mjini Leeds, Uingereza, amefichua kuwa matumizi ya muda mrefu ya paracetamol yana athari mbaya kiafya.
Professa Conaghan alipitia tafiti nane zilizofanyika huko nyuma kutathimini uhusiano baina ya matumizi ya muda mrefu ya paracetamol na matatizo ya kiafya kwa watu wazima.
Utafiti huo umebaini wagonjwa wanaopewa dawa hizo za kupunguza maumivu mwilini kwa muda mrefu wana hatari kubwa ya asilimia 63 kufupisha maisha yao.
Hatari ya kupatikana ugonjwa wa moyo na kiharusi iko juu kwa asilimia 68, huku pia kukiwa na hatari kubwa ya asilimia 50 ya kupatikana vidonda vya tumbo au hata kuvuja damu.
“Kwa kuegemea takwimu hizo hapo juu, tunaamini hatari halisi ya matumizi ya paracetamol kuwa ya juu kuliko inayodhaniwa na jamii ya wataalamu wa afya,” alisema.
Watafiti hao walihitimisha kuwa kutokana na ukubwa wa matumizi ya paracetamol na urahisi wa upatikanaji, uchunguzaji wa athari zinazoweza kupatikana kutokana na dawa hizo ulipuuzwa.
Professa Nick Bateman wa Chuo Kikuu cha Edinburgh, alisema wanadhani utafiti huo umetoa mwanga kuhusu matumizi ya muda mrefu ya paracetamol.
Anasema hata hivyo matumizi ya paracetamol hayapaswi kuachwa moja kwa moja.
Professa Bateman pia anashauri kuwa watu wanapaswa kutumia kiwango cha chini cha dozi ya paracetamol kwa kipindi kifupi ambacho kinaweza kuzuia matatizo ya kiafya.
Naye Professa Conaghan anakiri takwimu hizo zinaweza kuwatisha watu wanaotumia paracetamol kwa kipindi kirefu.
Hata hivyo, anasema watu wanapaswa kushauriana na madaktari wao au wataalamu wa afya kabla ya kutumia paracetamol kwa kipindi kirefu.
Watafiti wanasema utafiti huo ni muhimu kwa vile utawasaidia madaktari kuwashauri wagonjwa kuhusu hatari zilizopo iwapo watatumia dawa hizo kwa kipindi kirefu.

SLAA ANUSURIKA KIFO

 DAR ES SALAAM
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amenusurika kuuawa na mlinzi wake.
Hilo limebainika baada ya kitengo cha ulinzi cha chama hicho kutibua mpango unaodaiwa kuratibiwa na maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa (TIS), wa kumuua kiongozi huyo kwa kumtumia mlinzi wake binafsi (PSU), Khalidi Kagenzi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Mabere Marando, alisema Kagenzi akiwa mlinzi binafsi wa Dk. Slaa katika kipindi cha miaka miwili, amebainika kutumiwa na vyombo vya usalama vya nchi pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuvujisha siri za chama hicho, na kupewa kazi ya kumuua katibu huyo wa Chadema.
Akielezea tukio lililombaini mlinzi huyo, Marando alisema lilitokea Ijumaa iliyopita baada ya mashushushu wa chama hicho kumwona mlinzi huyo akipanda gari lenye namba za usajili T 213 ARS linalodaiwa kutumiwa na Ofisa Usalama wa Taifa wa Kinondoni.
“Baada ya kuonekana ndipo mashushu wa Chadema walichukua jukumu la kumkamata na kumfanyia mahojiano ambapo walifanikiwa kumpekua katika simu zake mbili zinazotumia mitandao ya Vodacom, Airtel na Tigo.
“Katika simu hizo, walikuta ujumbe mfupi wa maneno uliokuwa ukitoka kwa …, aliyempigia mara tatu na kumtumia fedha kati ya Desemba 4, mwaka jana na Julai 14, 2014. Namba nyingine zilizokutwa zilikuwa za maofisa Usalama wa Taifa,” alisema.
Aliongeza kuwa baada ya upekuzi huo katika ‘Note book’ na simu zake, waligundua kuwa kigogo mmoja wa ngazi za juu wa CCM alimtumia muda wa maongezi wa Sh 50,000 kwa namba ya simu 0764 …222 Julai 14, 2014 na Desemba 4, 2014 alimtumia Sh 150,000.
Marando alisema katika upekuzi wa kwenye simu, walibaini mazungumzo yake yote yalikuwa yakitumia muda usiopungua saa mbili hadi tatu, na mara zote ni wakati ambao Chadema walikuwa wakifanya mikutano yao ya ndani.
“Alikuwa akitumia simu yake kurekodi kila kilichokuwa kikizungumzwa kwenye mikutano yetu na kusambaza kwa CCM, na iligundulika akiwasiliana na maofisa wa Usalama wa Taifa waliofikia 22,” alisema.
Marando aliongeza kwa kusema kuwa kama isingekuwa suala la kutolewa kwa uhai wa Dk. Slaa, wasingezungumzia suala hilo na pia anazungumziwa huenda akachaguliwa kuwa mgombea wa urais wa Ukawa.
Alisema kuwa jana chama hicho kimetoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili kuchukua hatua za kisheria ambao ndio wanaweza kutaja majina ya maofisa usalama wa waliohusika na mpango huo.
Akijibu swali kutoka kwa waandishi wa habari kuhusu afya ya Dk. Slaa, alisema hadi jana alikuwa salama ingawa bado hajapima kubaini hilo.
Marando alisema baada ya kugundulika kufanya hujuma hizo, Ijumaa iliyopita walimsimamisha majukumu yake ya kumlinda kiongozi huyo hadi pale uchunguzi dhidi yake utakapokamilika.
Ingawa chama hicho hakikueleza kiasi cha fedha ambacho mtuhumiwa alipewa kufanyia shughuli hiyo, lakini kwa mujibu wa maelezo aliyoyatoa kwa Idara ya Ulinzi wa chama hicho, alionyesha ndani ya simu yake kiasi cha Sh milioni 7 ambazo zilikuwa muda wa maongezi kwa muda wa miaka miwili.
tulipomtafuta kigogo wa CCM aliyetajwa, hakupatikana ofisini kwake Lumumba wala Dodoma, na hata alipopigiwa simu yake ya mkononi iliita bila kupokewa.
Pamoja na jitihada hizo, pia alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu ‘SMS’ hakuweza kujibu hadi tunakwenda mitamboni.
Taarifa kutoka ndani ya Chadema zinaeleza kuwa tangu Ijumaa baada ya kugundulika kwa mpango huo walinzi wa chama hicho walikuwa wakimsulubu kwa kipigo Kagenzi ili kuweza kupata ukweli.
Huku akiwa anapigwa, Kagenzi
alilazimika kutaja majina ya watu wote waliokuwa wakifanya kazi hiyo ikiwamo kuandika taarifa maalumu ikiwamo shughuli binafsi za Dk. Slaa.
POLISI WAZUNGUMZA
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Camillus Wambura, alithibitisha kufikishwa mtuhumiwa huyo katika Kituo cha Polisi Oysterbay ambapo alisema wanaendelea na mahojiano naye ili kujua ukweli wa tuhuma zinazomkabili.
“Tumempokea leo (jana) mtuhumiwa, tumeanza kuwahoji waliomleta na baadaye kumhoji muhusika ili tuweze kubaini ukweli kuhusu tuhuma dhidi yake,” alisema Kamanda Wambura.

4 Mar 2015

TULLY AMJIBU JERRY MURO

Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Simba, Said Tully amesema mpira umeingiliwa kwa kuwa wanacholalamika Yanga ni sawa na kichekesho.

Ingawa hajawaweka wazi, Tully ameonyesha kulenga maneno yaliyozungumzwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Yanga, Jerry Muro aliyesema kuwa Simba ilimchezesha mshambuliaji Ibrahim Ajibu 'Kadra' katika mechi dhidi  ya Prisons.
"Nashangazwa sana na kauli, watu wanazungumza, hawajui lolote. Ili mradi tu wanasema, suala la Ajibu lilipitia taratibu zote viongozi wa Yanga wanajua.
"Sasa unasikia mtu anasema mambo ambayo yanashangaza kabisa kuonyesha hajui lolote kuhusu soka, nasema amevamia huku maana watu wa mpira tunajuana," alisema Tully.
Kabla, Muro alitoa malalamiko kuwa Simba ilimchezesha Ajibu ikijua ana kadi tatu za njano jambo si sahihi.

Lakini Simba ikatoa ufafanuzi kutumia kanuni mpya zinazoruhusu kuchagua mchezaji asicheze katika mechi ipi kutokana na uchaguzi wao.

Naye Msemaji wa TFF, Baraka Kizuguto akalifafanua hilo kwa kusema hakuna kosa lolote kwa kuwa mkutano wa pamoja wa viongozi wa klabu, TFF na Bodi ya Ligi ulipitisha kanuni hizo mpya.

JB KUANDAA FILAMU KUPINGA MAUAJI YA ALBINO


WAIGIZAJI wa filamu nchini, wanatarajia kuungana katika filamu moja itakayokuwa ikipinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).
Mwigizaji Jacob Steven ‘JB’, alizungumza na  hivi karibuni, wakati wa kongamano la amani lililoandaliwa na maaskofu na masheikh wa Mkoa wa Mwanza.
JB ambaye alikuwa ameongozana na wasanii wengine kama Mzee Majuto na Mrisho Mpoto, alisema mchakato wa kuandaa filamu hiyo umeanza.
“Tumeguswa na mauaji ya walemavu wa ngozi, ambayo yamekuwa yakitokea kila mara kanda ya ziwa, tutatengeneza filamu ambayo kila mtu akipata nafasi ya kuitazama itafikisha ujumbe wa kuacha kufanya mauaji,” alisema JB.
Kwa upande wake, Mzee Majuto, alisema umefika wakati suala la mauaji ya watu wenye ulemavu yakamalizika na kukomeshwa kabisa.

WOLPER AZAMA KWA DOGO WA MAKOMANDOO

Siri imefichuka! Bwa’mdogo a.k.a Serengeti Boy kutoka Kundi la Makomando, Fredy Felix amesimulia namna alivyofaidi penzi la staa wa Bongo Movies, Jacqueline Walper Massawe ‘Wolper’.
Akizungumza  kwenye mahojiano maalum juzikati, dogo huyo alisema kuwa katika maisha yake ya kimapenzi hakuna mwanamke ambaye aliwahi kutoka naye na kujiachia kwa furaha kama ilivyo kwa Wolper.
“Kiukweli msichana pekee ambaye nimewahi kuwa naye katika mapenzi na kumpenda kwa dhati ni Wolper pekee.“Mara yangu ya kwanza kukutana naye ilikuwa kama ‘sapraiz’ vile (habari zinasema kwamba walikutana maeneo ya Kinondoni), alipoingia kwangu nashukuru naye alinipenda na kunifanyia kila nilichohitaji.
“Nampenda sana Wolper na kila siku nimekuwa nikiahidi kwamba huyo ndiye mwanamke pekee ambaye nitakuja kuishi naye hata kama ni uzeeni maana ninampenda kutoka moyoni.“Sidhani kama moyo wangu utampenda mwanamke mwingine kama nilivyompenda Wolper. Kiukweli niliinjoi sana penzi lake,” alisema Fredy huku akijutia kumwagana naye bila sababu ya msingi.
Alipotafutwa Wolper ili kupata undani wa ishu hiyo simu yake ilipokelewa na aliposomewa mashtaka yake alikaa kimya bila kujibu chochote. Hata hivyo jitihada za kumtafuta zinaendelea.

GWAJIMA APEWA NOTICE

NI msala! Kupigwa notisi ya kutakiwa kuhamisha kanisa kwa  Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kumeelezwa kusaba

bishwa na baadhi ya makahaba, wavuta bangi na wengineo.

Mapema wiki iliyopita, Gwajima amepewa  notisi na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ikimtaka kuhamisha kanisa lake kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar ifikapo Machi 9, mwaka huu.
Taarifa i zinasema kuwa, barua mbili za NHC zilipelekwa kwa makanisa  mawili likiwemo la Ngurumo ya Upako la Nabii George David ‘Geor Dave’ (Amani lina nakala).
Amani lilifika kwenye viwanja  hivyo mwanzoni mwa wiki hii na kuzungumza na wenyeji wa eneo hilo ambao walisema hata wao wanasikia mchungaji huyo anatakiwa kuondoka eneo  hilo lakini kwa ajili ya kupisha ujenzi wa nyumba za NHC.
Katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mzimuni, Amani lilizungumza na mwenyekiti wake,  Hassan Faraji Nganyani ambapo alikiri kupata kopi ya barua hiyo.
“Ni kweli ndugu waandishi kopi ya barua kutoka Shirika la Nyumba la Taifa tumepata, inawataka viongozi wa  makanisa  hayo mawili kuhama ifikikapo Machi 9, mwaka huu,” alisema kiongozi  huyo.
Kiongozi huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, kuhamisha makanisa hayo ili kujenga nyumba za shirika ni sahihi lakini tatizo jingine ni kwamba, siku ambazo waumini hao hawakeshi  kanisani hapo, kuna  makundi  ya watu hufika eneo hilo na kufanya ukahaba, wengine  kutupa vichanga baada ya kutoa mimba achilia mbali wahuni wanaovuta bangi na mateja mbalimbali ‘wabwia unga’.
Mzee mmoja ambaye alisema ni mstaafu wa serikali alisema kuwa, alishapeleka maombi kwenye shirika la nyumba akitaka eneo hilo lidhibitiwe baada ya baadhi ya watu, ukiacha makanisa kulitumia vibaya.
“Ni kweli siku kukiwa hakuna ibada, wahuni, malaya, wavuta bangi na watumia madawa ya kulevya wanageuza maskani yao. Nadhani NHC walizingatia pia maombi yangu na ya wengine,” alisema mstaafu huyo.
Waandishi walifakiwa kuongea na baadhi ya watu wanaoabudu  katika Kanisa la Gwajima ambapo walisema eneo hilo lilikuwa  limezoeleka kwa kila mtu aliyekuwa  akiabudu hapo.Baadhi yao walisema uwanja huo ulikuwa  unatosheleza  umati  uliokuwa ukifika kusikia Neno la Mungu lakini baada  ya kupata  notisi hawajui  watapata wapi  kiwanja  kikubwa kama hicho.
Juhudi za kumpata Mchungaji Gwajima hazikufua dafu baada ya simu yake kuita muda mrefu bila kupokelewa. Amani lilipofika kanisani kwake ilidaiwa yuko safarini.
Mchungaji Gwajima alihamia katika viwanja hivyo mwaka 2008 akitokea Ubungo Chai Bora, Dar ambako kulionekana kutokidhi idadi ya watu.Nabii Geor Dave naye alipotafutwa na Amani kwa njia ya simu hakupatikana hewani hadi gazeti linakwenda mitamboni.

SAKATA LA WEMA KAJALA LAFIKIA PATAMU

Kwa hatua lilipofikia bifu zito kati ya mastaa mashosti wa zamani, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Kajala Masanja ‘Kay’, imebainika kwamba hakuna ambaye yupo tayari kumzika mwenzake.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa waigizaji hao, mtafaruku huo umechukua sura mpya mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya Madam kuanika ubaya aliotendewa na Kajala aliyewahi kumlipia faini ya shilingi milioni 13 na kumuepusha na kifungo cha miaka 7 jela, Machi 25, 2013.
“Hali ni tete, Madam ameibua bifu upya alipofunguka kupitia kipindi chake cha In My Shoes kinachorushwa na Runinga ya EATV, hapo ndipo ilipodhihirika kwamba wawili hao hawawezi kuzikana wala kusameheana.
TIMU KAJALA WAJA JUU
“Wafuasi wa Kajala hawakufurahishwa na maneno ya Wema ambayo walidai yalikuwa na lengo la kumvua nguo mwenzake, yale matumaini ya kusameheana hayapo tena, ni bifu hadi wanakwenda kaburini,” kilisema chanzo hicho.
WEMA ALIFUNGUKA NINI?
Kwenye kipindi hicho, mbali na mambo mengine, Wema alieleza kuwa Kajala hakuwahi kuwa rafiki yake lakini alijitolea kumlipia faini kumuepusha na kifungo kutokana na kuguswa na kuingiwa na moyo wa huruma kama msanii mwenzake.
“Sikuwahi kuwa na urafiki na Kajala, kilichonifanya niwe karibu naye ni mwanaye ambaye alikuwa akinipenda na kutaka kukutana na mimi...,” alisema Madam.

Kupitia kipindi hicho, Wema pia alizungumzia kiini cha ugomvi wao ambapo alianika kinagaubaga kwamba alichukizwa na suala la Kajala kumsaliti kwa kutembea na mchumba wake aitwaye CK (yule kigogo aliyesumbua mjini kwa kutapanya fedha).“Kajala hana fadhila, huwezi amini mtu ambaye niliamua kujitolea kwa moyo wangu kumlipia Sh. milioni 13 huyohuyo aje kutembea na mchumba wangu, huku ni kukosa ubinadamu kulikopitiliza,” alisema Wema.
TIMU KAJALA  WAMCHANA WEMA
Saa chache baada ya Wema kufunguka, wafuasi wa Kajala mitandaoni walimjia juu Wema kwa kumwambia kuwa hana busara na ndiyo maana ameamua kutamka maneno hayo waliyoyaita kuwa ‘ni ya aibu’.
“Wema hana busara, mtu mwenye busara zake hawezi kuzungumza hadharani mambo ya kuibiana mabwana, ni ujinga tu. Unazungumza ili iweje?” aliandika mfuasi wa Kajala mtandaoni.
KAJALA AFURA
Jitihada za kumpata Kajala aweze kuzungumzia mashambulizi hayo ya Wema hazikuzaa matunda baada ya simu yake kuita bila kupokelewa lakini shosti yake wa karibu alisema Kajala amechukizwa na maneno hayo ya Wema na kamwe hatakuja kukaa naye meza moja, achilia mbali kumzika.

KUELEKEA MECHI YA WATANI WAJADI

Kocha wa Simba, Goran Kopunovic ameamua kuwapumzisha wachezaji wake kesho.

Wachezaji wa Simba watafanya mazoezi kesho jioni baada ya mazoezi makali ya leo visiwani Zanzibar.

SAFARI YA MWISHO YA KOMBA

Safari ya mwisho ya mbunge wa Mbinga Magharibi jana ilihitimishwa saa 9.25 alasiri wakati mwili wake ulipofunikwa na mfuniko mkubwa wa zege uliobebwa na gari maarufu kwa jina la “kijiko”.
Haikuwa kitu cha kawaida wakati gari hilo kubwa likishusha mfuniko huo wa zege kwenye kaburi la mwimbaji huyo maarufu wa nyimbo za uhamasishaji za CCM na kiongozi wa kundi la Tanzania One Theatre (TOT), lakini majonzi yaliwafanya waombolezaji kulichukulia tukio hilo kuwa la kawaida.
Safari ya Komba, iliyoanza miaka 61 iliyopita kwenye kijiji cha Lituhi ambako aliazikwa jana, ilikamilishwa kwa salamu mbalimbali ambazo zilielezea ushupavu wa kapteni huyo mstaafu wa jeshi.
Mazishi hayo yaliyohudhuriwa na mamia ya wananchi, wakiwamo viongozi mbalimbaliwakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete na mkewe Salma, yalifanyika katika makaburi ya Misheni,katika Kijiji cha Lituhi (Bundi) wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.
Nyuso za majonzi zilitawala kwa waombolezaji waliojitokeza nyumbani kwa marehemu, takriban mita 500 kutoka katika makaburi hayo na baadaye katika misa iliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Lituhi, ikiongozwa na Askofu John Ndimbo wa Jimbo Katoliki la Mbinga.
Kaimu katibu wa Bunge, John Joel, akisoma wasifu wa marehemu, alisema Kapteni Komba aliyefariki dunia Februari 28, mwaka huu akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam, alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya shinikizo la damu na mara kadhaa Ofisi ya Bunge ilimpeleka India kwa matibabu. Pia alikuwa na tatizo la kisukari ambalo ndilo lililochukua maisha yake.
Mazishi hayo yalishuhudiwa na viongozi mbalimbali, akiwamo Edward Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Utaratibu na Bunge), Jenister Mhagama na mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi.
Wengine ni Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Ali Abdallah Ali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya na Spika wa Bunge, Anne Makinda.

3 Mar 2015

MZEE MAKAMBA ASHINDWA KUJIZUIA

Katibu Mkuu wa CCM mstaafu Mzee Yusuph Makamba akilia wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu John Komba.

RAIS ANAYEMALIZA MUDA WAKE APATA TUZO

RAIS anayemaliza muda wake nchini Namibia, Hifikepunye Pohamba, ameshinda tuzo ya Mo Ibrahim inayotolewa kwa kiongozi wa Afrika aliyeonyesha uongozi bora.
Tuzo hiyo yenye thamani ya dola za Marekani milioni tano (sawa na Sh bilioni 9.2 za Tanzania) ni kubwa zaidi duniani kutolewa kwa mtu mmoja mmoja.
Fedha hizo hutolewa kila mwaka kwa kiongozi wa kuchaguliwa aliyetawala vizuri kwa kuinua viwango vya maisha ya raia wake na kisha kuondoka madarakani kwa amani.
Lakini mwaka jana tuzo hiyo ilikuwa ya nne kwa kipindi cha miaka mitano kukosa mshindi.
Pohamba, mpiganaji wa zamani wa waasi aliyepigania uhuru wa nchi yake, alitumikia mihula miwili kama rais wa Namibia.
Alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2004, na mara nyingine mwaka 2009. Nafasi yake inatarajiwa kuchukuliwa na Rais mteule, Hage Geingob.
Pohamba alikuwa mwanachama mwanzilishi wa South West Africa People’s Organisation (SWAPO), vuguvugu la msituni lililoendesha harakati za miongo mingi ya kupigania uhuru dhidi ya Afrika Kusini.
Tangu ipate uhuru mwaka 1990, SWAPO imetawala siasa za nchi hiyo ikishinda kwa wingi wa kura katika uchaguzi. Mo Ibrahim ni Mwingereza mwenye asili ya Sudan, mhisani na mfanyabiashara wa sekta ya mawasiliano ambaye alijitengenezea mabilioni ya fedha kwa kuwekeza Afrika.

ZITO AMTOLEA UVIVU CHENGE



WAKATI Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma ikiendelea na mvutano wa sheria na Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, amesema mbunge huyo alistahili kufungiwa kushiriki kwenye uongozi wa umma muda mrefu.
Zitto aliliambia Mtanzania kuwa tangu izuke kashfa ya rada ambayo pia Chenge alihusishwa, tume ya maadili ilipaswa kumuhoji na kumchukulia hatua kali za sheria.
“Chenge kwa mara ya pili sasa anaonekana kuwa ana makosa ya maadili. Kwenye rada taratibu kama hizi za sasa hazikufanyika. Ilipaswa zifanyike aeleze alipata wapi fedha alizoziita vijisenti, alizoweka huko kwenye visiwa vya Jersey.
Jambo hilo lilipita tu bila Baraza la Maadili kulifanyia kazi, wanachofanya sasa Baraza la Maadili kwenye Escrow ndiyo ilipaswa ifanyike kabla kiasi kwamba Chenge asingekuwa kwenye uongozi wa umma.
Katiba ipo wazi inasema mtu anaweza kupoteza ubunge kwa makosa ya maadili.
Zitto alisema kinachoendelea kwenye baraza hivi sasa ni funzo kubwa na kufumbua macho kwamba mfumo wa kushughulikia maadili upo isipokuwa haukuwezeshwa kufanya kazi.
Sasa tuuwezeshe uweze kushughulika na kesi za utovu wa maadili.
Swali: Ni kipi kilichofanya sasa baraza lichukue hatua?
Jibu: Baraza limeibuka kwa sababu kuna hasira za wananchi kuhusu Escrow. Hasira zilizokitisha Chama cha Mapinduzi kwa kiwango cha kuanza kuchukua hatua.
Hasira hizi hazikuweza kuelekezwa vizuri kwenye kashfa ya rada na kashfa nyingine. Sasa wananchi wanadai viongozi wanaoshutumiwa kwa ukwasi mkubwa tofauti na kipato chao wachunguzwe na waitwe mbele ya baraza kujieleza. Itasaidia kurejesha imani ya wananchi kwa uongozi wa umma.
Mbali na suala hilo, kwenye ukurasa wake wa Facebook, Zitto jana alisema Maadili ya Viongozi wa Umma ni moja ya mjadala mkubwa Uingereza hivi sasa.
“Wabunge waandamizi wawili, Jack Straw na Malcolm Rifkind, wamekutwa na kashfa kubwa ya kutumia ubunge wao kuishawishi kampuni binafsi kuhusu malipo,” alisema.
Alisema wabunge hao wameamua kung’atuka kwa aibu kubwa.
“Suala kama hili linatokea sana Tanzania ambako hakuna kanuni za maadili za wabunge – kuna Azimio la Bunge la mwaka 2004 kutunga kanuni hizi lakini hakuna lililofanyika. Niliwasilisha muswada binafsi kuweka kanuni hizi ukafanyiwa mizengwe.
“Wabunge wa Tanzania kutumia nafasi zao kushawishi kwa maslahi ya makampuni binafsi na kulipwa kwa kazi hiyo ni jambo la kawaida,” alisema.
Alisema kuna mbunge anatumia nafasi yake kutoa matangazo ya biashara kwenye gazeti lake yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 200 kwa mwaka.
“Kuna Mbunge ana gazeti linalotoka wakati wa Bunge la Bajeti tu kwa ajili ya kupata matangazo. Wengine wana zabuni za Bunge.
“Wabunge takribani wote ni wafaidika wa misamaha ya kodi ama kwa mujibu wa stahili zao au kwa kutumia ushawishi wao kupata misamaha ya biashara wanazofanya,” alisema.
Alisema Chama cha Labour cha Uingereza kimeweka katika Ilani yake ya Uchaguzi kwamba wabunge wote wa chama hicho ni marufuku kufanya kazi nyingine wakiwa wabunge na kuwa kikishika madaraka kitatunga sheria kuzuia wabunge kufanya kazi nyingine.
Wiki hii huenda ikawa ngumu kwa Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (CCM), pamoja na watumishi mbalimbali wa Serikali ambao wanatarajiwa kusimama mbele Baraza la Maadili kwa ajili ya kusomewa mashtaka ikiwamo kupokea mgao wa fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow.
Februari 23 mwaka huu, alihojiwa Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka (CCM) na uamuzi yunatarajiwa kutolewa Machi 13 mwaka huu.
Hata hivyo, Mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge (CCM) aligoma kuhojiwa na baraza hilo na kuamua kukata rufaa Mahakama Kuukwa kupata tafsiri ya neno zuio.

HATARIII

Mazoezi anayofanya huyu jamaa acha kabisa

AZAM WALIANZISHA LA TIMUA TIMUA

Kipigo cha mabao 3-0 ugenini dhidi ya El-Merrikh ya Sudan, kimemponza kocha Joseph Omog baada ya uongozi wa Azam FC kuamua kumtimua.
Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa facebook wa Azam FC muda mfupi uliopita, Uongozi wa Azam FC umetangaza kumtimua raia huyo wa Cameroon.
Taarifa hiyo inasomeka: “Uongozi wa Azam FC unatangaza kuachana na kocha wake mkuu Joseph Omog baada ya kuwa naye kwa miezi 14.
Omog aliyeipa Azam FC ubingwa wa kwanza msimu uliopita ameondoka pamoja na msaidiI wake Ibrahim Shikanda.
Kwa sasa timu itakuwa chini ya George Best Nsimbe.”

YANGA NA REKODI YAKUTOFUNGWA



Yanga SC hawajapoteza mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya mahasimu wao Simba SC kwa msimu wa tatu sasa, na mchezo ujao wa ‘ Dar es Salaam derby’ siku ya Jumapili ijayo utakuwa ni mchezo wa sita. Mara ya mwisho Simba kuishinda Yanga katika ligi kuu ni Mei 7, 2012 walipochomoza na ‘ ushindi mkubwa zaidi katika karne’ . Simba ilishinda mabao 5-0 msimu ambao walitwaa ubingwa wao wa mwisho katika ligi kuu.

Yanga imeifunga Simba mara moja tu katika michezo mitano iliyopita ya ligi kuu na wataingia kwa mara ya sita mfululizo ‘ wakiwa katika umbo la ushindi’ siku ya Jumapili ili kukamilisha msimu wa tatu pasipo kufungwa na mahasimu wao hao katika ligi kuu.  Msimu wa 2012/13 timu hizo ‘ watani wa jadi’ zilifungana bao 1-1 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, kisha Yanga ikaishinda Simba kwa mabao 2-0, Mei, 2013 na kutwaa ubingwa wao wa 24.
Msimu wa 2013/14 timu hizo zilitengeneza ‘ mchezo wa aina yake’, Oktoba, 2013. Yanga walimaliza dakika 45 za kwanza wakiwa katika kiwango cha juu huku wakiwa mbele kwa mabao 3-0, kufikia dakika ya mwisho ya mchezo huo Simba ‘ walikomboa’ magoli yote na kutengeneza sare ya 3-3. Katika mchezo wa marejeano siku ya mwisho ya msimu, April 24, 2014 Yanga walisawazishia kupitia kwa Saimon Msuva zikiwa zimesalia dakika chache mchezo kumalizika na kutengeneza sare ya kufunga bao 1-1.
Oktoba, 2014 timu hizo zilitengeneza sare ya nne mfululizo katika ligi kuu baada ya kumaliza dakika 90 bila kufungana. Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza msimu huu Yanga waliingia uwanjani wakiwa na matumaini makubwa ya kushinda lakini wakajikuta wakibanwa mbavu na Simba ambayo ilianza na wachezaji sita kutoka timu yao ya pili.
Patrick Phiri ndiye mwalimu wa mwisho wa Simba kuikabili Yanga katika ligi kuu. Phiri alitimuliwa klabuni hapo mara baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Kagera Sugar mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka jana. Nafasi ya Mzambia huyo kwa sasa ipo chini ya Mserbia, Goran Kopunovic. Goran hajawahi kushiriki katika mchezo wa ‘ Dar es Salaa Pacha’, baada ya kufanya kazi Rwanda na Vietnam, Goran atakutana na presha kubwa katika mchezo wa ‘ tatu kwa ukubwa barani Afrika’. Mchezo ambao mashabiki huzimia na wengine hupoteza maisha kwa bahati mbaya kutokana na presha.
Marcio Maximo ndiye mwalimu wa mwisho kuifundisha Yanga katika ligi kuu, mkufunzi huyo raia wa Brazil alitimuliwa kazi mara baada ya Yanga kufungwa na Simba mabao 2-0 Disemba, 2014 katika mchezo wa hisani wa ‘ Nani Mtani Jembe-2’. Lakini katika ligi kuu kocha huyo aliendeleza kutunza rekodi ya Yanga kutofungwa na Simba tangu waliporuhusu kipigo kikubwa cha mabao 5-0 miaka mitatu iliyopita. Maximo ndiye mwalimu aliyeiongoza Yanga katika suluhu ya 0-0 Oktoba mwaka jana.
Hans tayari anajua presha ya SIMBA NA YANGA kwa kuwa tayari alishawahi kuiongoza Yanga kusawazisha katika mchezo wa mwisho wa msimu uliopita. Ni kocha ambaye ameifanya Yanga kuwa na mchezo wa kushambulia na kufunga mabao. Kumbuka Yanga haifungwa na Simba katika ligi katika michezo mitano mfululizo huku wakishinda mara moja. KUELEKEA ‘ Dar es Salaam derby ‘ Jumapili hii niteendelea kukuletea rekodi zinazocheza kuhusu mahasimu hao. Kesho tutatazama ‘ Mbinu na ufundi wa makocha’

KOMBA AWALIZA KIKWETE, MAKINDA

RAIS Jakaya Kikwete amewaongoza mamia ya wananchi wa Jiji la Dar es Salaam, wabunge, viongozi wa Serikali na wanasiasa wengine kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba, huku akisema kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe ni pigo.
Amesema kifo cha Kapteni Komba kimeliondolea Taifa mmoja wa viongozi wake wazuri, msanii mahiri, raia mwema na mzalendo wa kweli.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana, Rais Kikwete alisema: “Wakati tulipokuwa tunajiandaa kurekodi hotuba hii tukapata habari ya huzuni na majonzi makubwa ya kifo cha Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba.
“Marehemu alitumia muda mwingi wa maisha yake kuelimisha jamii kuhusu mambo mema, amefanya hivyo akiwa mwalimu na baadaye kiongozi wa kikundi cha sanaa cha JWTZ na hapa mwishoni kiongozi wa kikundi cha Tanzania One Theatre cha Chama Cha Mapinduzi.
“Kwa kutumia kipaji alichojaaliwa na Mola wake, ametoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi yetu na ustawi wa chama tawala. Daima tutamkumbuka kwa mambo mengi mema aliyoifanyia jamii ya nchi yetu na taifa kwa jumla.”
Rais Kikwete aliwataka Watanzania wote kuungana na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu.
Kutokana na msiba huo, aliwataka wananchi wa Jimbo la Mbinga Magharibi kutambua namna bora ya kumlilia mbunge wao aliyewapenda, ikiwamo kudumisha mema aliyoyafanya na kukamilisha kazi alizokusudia kuzifanya.
“Kwa familia ya ndugu yetu mpendwa, napenda kuwahakikishia kuwa tuko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na maombolezo.
“Tunawaombea kwa Mola awape moyo wa subira na uvumilivu. Wananchi wa Wilaya ya Nyasa tunawapa pole nyingi kwa msiba mkubwa uliowakuta na pengo kubwa mlilolipata,” alisema mkuu huyo wa nchi.
MAKINDA
Kabla ya shughuli ya kuaga mwili wa marehemu kuanza, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alitumia fursa ya kutoa salamu za rambirambi kumwombea marehemu msamaha kwa umma kama kwa namna yoyote ile aliwakwaza.
Alisema kufariki dunia ghafla kwa Kapteni Komba ni sawa na moto wa kibatari, unavyoweza kuzimika wakati wowote.
“Kwa kuonyesha kwamba kifo hakina taarifa, na Mungu anavyotaka ndivyo inavyokuwa, ndiyo maana hata Jumamosi marehemu bado alikuwa akiendelea kuandika baadhi ya nyimbo zake.
“Ninaamini kama marehemu angepewa robo saa kabla ya kifo chake angesema maneno haya: ‘naomba msamaha kwa yeyote niliyemkosea’. Kwa sababu yeye ni binadamu, katika shughuli zake yawezekana kabisa kuna watu aliwakwaza, kwahiyo kama kuna mtu alimkosea, tumsamehe,” alisema Spika Makinda.
Alisema si vyema kwa baadhi ya watu kuendelea kumsema kwa mabaya marehemu.
“Baada ya kutokea kifo cha Kapteni Komba, baadhi ya watu wamekuwa wakitoa kauli za kumlaumu kwa maelezo kuwa wakati wa Bunge la Katiba, alizungumza maneno ambayo yaliwakwaza baadhi ya watu. Hili si sawa ndugu zangu,” alisema.
NYIMBO ZALIZA WATU
Wakati wa kuaga mwili wa marehemu Kapteni Komba, wasanii mbalimbali waliimba nyimbo maalumu ambazo ziligusa hisia za waombolezaji ambapo muda wote walikuwa wakibubujikwa machozi.
Mbali na wananchi wa kawaida, baadhi ya viongozi akiwamo Rais Kikwete na Spika Makinda, walishindwa kujizuia na kujikuta wakimwaga machozi.
Moja ya nyimbo zilizowagusa viongozi hao, ni ule ulioimbwa na wasanii wa dansi wakiongozwa na mkongwe King Kikii.
Kipande cha wimbo huo ambacho Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye alighani, ndicho kilionekana kuwagusa wengi.
Baadhi ya maneno ya kipande hicho ni; ‘Komba akifika huko anakokwenda, amweleze Baba wa Taifa hali ya nchi ilivyo kwa sasa’.
KINANA
Akitoa salamu za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alisema kishindo cha kifo cha mwanasiasa huyo ambaye pia ni msanii maarufu, kimezima sauti yake maarufu iliyojulikana na takribani Watanzania wote.
“Sauti zetu huzimwa na roho zikasimama kwa matakwa ya Mungu,” alisema Kinana.
Alisema huwezi kuzungumzia kukua na kuchanua kwa CCM bila kumtaja Komba aliyekuwa mkuu wa Idara ya Sanaa ya chama hicho, kwani nyimbo zake zilichangamsha wengi.
“Kwenye vita vya Kagera alikuwa anawahamasisha askari wetu, kwenye msiba wa Baba wa Taifa (Mwalimu Julius Nyerere) aliwafariji Watanzania, kifo chake ni pengo kubwa kwa CCM,” alisema Kinana.
NASSARI
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari (Chadema), aliyemwakilisha Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, alisema pamoja na tofauti za kiitikadi, Kapteni Komba alimuheshimu bila kujali chama alichokuwa akitokea.
“Tumekuwa pamoja na Kapteni Komba katika kamati na wala hakuwahi kujali tofauti ya itikadi zetu za vyama, hasa linapokuja suala la taifa.
“Neno la faraja ambalo ningependa kuwaacha nalo ni lile lililo kwenye kitabu cha Zaburi linalosema; ‘Nitainua macho yangu nitazame milima, msaada wangu huu katika Bwana aliyezifanya mbingu na nchi’,” alisema.
SAID MTANDA ASIMULIA
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Said Mtanda, alisema Februari 24, mwaka huu alizungumza na Kapteni Komba kuhusu safari ya kamati waliyokuwa wanatarajia kusafiri kwenda nchini Ethiopia.
“Ilipofika Machi Mosi saa 10 nilipigiwa simu ya kuelezwa kwamba Komba ameaga dunia. Nilihuzunika kwa sababu alikuwa amana ya Serikali, chama, Bunge, jimbo lake la Mbinga Magharibi na wasanii aliokuwa akiwalea pamoja na Watanzania,” alisema.
Mtanda aliongeza kuwa ucheshi wa Kapteni Komba kwa wasanii na Watanzania, ulimfanya apachikwe jina la ‘Mlezi wa wana’.
Alisema uwezo wake na uzoefu ulichangia kubakishwa katika Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii kwa muda wa miaka tisa, hali iliyomfanya kuchaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa kamati hiyo hadi kifo kilipomkuta.
Alimmwagia sifa Kapteni Komba kwa kusema alisaidia kuimarisha CCM, alitetea haki za wazee ili wapate matibabu bure na alipambana kutetea mswada wa habari.
Alisema pamoja na hivi sasa dunia kupambana katika mazingira, lakini Komba alipambana katika uhifadhi wa mazingira tangu mwaka 1984 kwa kuhamasisha upande wa Tanzania Bara na visiwani Zanzibar.
YUSUFU MAKAMBA
Akimzungumzia Komba, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Yusufu Makamba, alisema kuwa anaamini ameumizwa zaidi na msiba huo kuliko mtu mwingine.
“Nimefanya kazi na Kapteni Komba kwa miaka sita nikiwa Katibu Mkuu, nimefanya naye kazi sehemu mbalimbali ikiwamo kwenye uchaguzi mdogo ukiwamo wa Tarime,” alisema.
Alisema Komba alikuwa amana ambayo ililetwa na Mungu kwa ajili ya CCM, hivyo anaamini atakiletea chama mwimbaji mwingine mwenye uwezo kama wake.
“Naamini Mungu atatuletea mwimbaji mwingine ambaye atakuwa mzuri ingawa hatamfikia Komba, kwani siku zote jino la dhahabu haliwezi kuwa kama la fedha,” alisema Makamba.
PURUKUSHANI KUAGA MWILI
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, umati wa wananchi ulifurika katika viwanja vya Karimjee kutaka kushuhudia safari ya mwisho ya Kapteni Komba, ambapo kila mmoja alitaka kutoa salamu zake za mwisho kwa kupita mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu.
Hali hiyo iliwapa wakati mgumu waandaaji wa shughuli hiyo jambo lililofanya askari maalumu wa Bunge kuingilia kati na kupanga watu ili wote waweze kutoa heshima zao za mwisho.
Wananchi hao walipata fursa ya kuaga mwili huo baada ya Rais Kikwete, wabunge na viongozi wa chama na Serikali kutoa heshima zao za mwisho.
Kundi la mwisho kutoa heshima lilikuwa ni familia ya marehemu ambapo hisia na vilio vyao, vilifanya waombolezaji wengine kushindwa kujizuia.
Mara baada ya kuagwa, mwili huo ulisafirishwa kwa ndege kwenda mkoani Ruvuma ambako wananchi walipata fursa ya kuuaga katika uwanja wa michezo wa Majimaji mjini Songea.
VIONGOZI WALIOHUDHURIA
Baadhi ya viongozi waliohudhuria ni pamoja na Rais Kikwete na mkewe Salma, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilali na wake zake, Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na mkewe Sitti, Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na mkewe Anna, Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa na mkewe.
Wengine ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Spika Anne Makinda, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ali Abdallah Ali, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
Wengine ni Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju, Jaji Kiongozi, Shaban Ali Lila, Spika mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi.
Pia walikuwapo Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Adam Kimbisa, mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Wengine ni Mwenyekiti wa Chama cha TLP na Mbunge wa Vunjo, Augustino Mrema, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Hussen Katanga pamoja na mwanasheria wa kujitegemea Hashimu Rungwe.