Taarifa ambayo kwanza ilianza kuenea
kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ajali ya basi la abiria na lori la
mizigo,kwamujibu wa mashuhuda kutoka
eneo la Changarawe, Iringa ambapo wamesema ni kweli ajali hiyo imetokea
na kuna idadi kubwa ya watu ambao wamefariki.
Mashuhuda wamesema basi la Majinja
lilitokea Mbeya kuja Dar es Salaam limegongana na lori la mizigo katika
eneo hilo, abiria waliofariki ni wengi japo idadi kamili haijafahamika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, kwa sasa yuko njiani kuelekea
eneo la tukio ili kuona mazingi
ra ya ajali na kutoa taarifa kamili
kuhusu ajali hiyo zitakujia kadri tutakavyo kuwa tukipokea.
No comments:
Post a Comment