Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe jana aliugua ghafla akiwa katika maandamano ya kumsindikiza
mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, Edward Lowassa baada ya
kuchukua fomu za kugombea urais katika Tume ya Taifa Uchaguzi (NEC).
Mbowe
alishiriki katika maandamano yaliyoanzia Makao Makuu ya CUF yaliyopo
Buguruni wilayani Ilala kuelekea NEC na baada ya Lowassa kuchukua fomu,
mwenyekiti huyo aliendelea na msafara kwenda Kinondoni yalipo makao
makuu ya Chadema.
Wakiwa njiani Mbowe na Mwanasheria
Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu walikuwa wamechomoza kwenye gari
wakiwapungia wananchi waliojitokeza kwenye maandamano hayo.
Hali
ya Mbowe ilibadilika ghafla na aliamua kushuka juu ya gari na kukaa
katika kiti, ndipo Lissu na watu waliokuwamo kwenye gari hilo wakaanza
kumpatia huduma ya kwanza kwa kumfungua vifungo vya shati lake katika
eneo la Kinondoni kwa Manyanya.
Wakati hali ya Mbowe
ilipoanza kubadilika msafara wa Lowassa ulikuwa ukielekea katika Uwanja
wa Biafra, Kinondoni na magari yalikuwa yakitembea mwendo mdogo kutokana
na maelfu ya watu waliokuwa wakiandamana.
Wakati
maandamano hayo yakiendelea, gari lililombeba Mbowe likiwa na walinzi wa
Chadema walioning’inia milangoni, lilichomoka katika msafara huo ambao
ulikuwa umeingia Barabara ya Kawawa na lilikunja kona katika barabara ya
kuelekea Mahakama ya Kinondoni kwa ajili ya kumwahisha hospitali na
taarifa zilizopatikana baadaye zilieleza kuwa lilielekea katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Akizungumzia hali hiyo, Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, alisema kuwa Mbowe yuko salama na anaendelea vizuri.
“Ni uchovu, uchovu, uchovu tu but he is out of danger (hayuko katika hali ya hatari),” alisema Lissu.
Ofisa
Uhusiano wa MNH, Aminiel Aligaesha alisema walimpokea Mbowe saa 11
jioni na alikuwa anaendelea na matibabu katika hospitali hiyo, hata
hivyo hakutaka kuweka wazi ugonjwa uliokuwa unamsumbua

No comments:
Post a Comment