Kwa hatua lilipofikia bifu zito kati ya mastaa mashosti wa zamani, Wema
Isaac Sepetu ‘Madam’ na Kajala Masanja ‘Kay’, imebainika kwamba hakuna
ambaye yupo tayari kumzika mwenzake. Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa waigizaji hao, mtafaruku huo umechukua sura mpya mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya Madam kuanika ubaya aliotendewa na Kajala aliyewahi kumlipia faini ya shilingi milioni 13 na kumuepusha na kifungo cha miaka 7 jela, Machi 25, 2013.
“Hali ni tete, Madam ameibua bifu upya alipofunguka kupitia kipindi chake cha In My Shoes kinachorushwa na Runinga ya EATV, hapo ndipo ilipodhihirika kwamba wawili hao hawawezi kuzikana wala kusameheana.
TIMU KAJALA WAJA JUU
“Wafuasi wa Kajala hawakufurahishwa na maneno ya Wema ambayo walidai yalikuwa na lengo la kumvua nguo mwenzake, yale matumaini ya kusameheana hayapo tena, ni bifu hadi wanakwenda kaburini,” kilisema chanzo hicho.
WEMA ALIFUNGUKA NINI?
Kwenye kipindi hicho, mbali na mambo mengine, Wema alieleza kuwa Kajala hakuwahi kuwa rafiki yake lakini alijitolea kumlipia faini kumuepusha na kifungo kutokana na kuguswa na kuingiwa na moyo wa huruma kama msanii mwenzake.
“Sikuwahi kuwa na urafiki na Kajala, kilichonifanya niwe karibu naye ni mwanaye ambaye alikuwa akinipenda na kutaka kukutana na mimi...,” alisema Madam.
Kupitia
kipindi hicho, Wema pia alizungumzia kiini cha ugomvi wao ambapo
alianika kinagaubaga kwamba alichukizwa na suala la Kajala kumsaliti kwa
kutembea na mchumba wake aitwaye CK (yule kigogo aliyesumbua mjini kwa
kutapanya fedha).“Kajala hana fadhila, huwezi amini mtu ambaye niliamua
kujitolea kwa moyo wangu kumlipia Sh. milioni 13 huyohuyo aje kutembea
na mchumba wangu, huku ni kukosa ubinadamu kulikopitiliza,” alisema
Wema.TIMU KAJALA WAMCHANA WEMA
Saa chache baada ya Wema kufunguka, wafuasi wa Kajala mitandaoni walimjia juu Wema kwa kumwambia kuwa hana busara na ndiyo maana ameamua kutamka maneno hayo waliyoyaita kuwa ‘ni ya aibu’.
“Wema hana busara, mtu mwenye busara zake hawezi kuzungumza hadharani
mambo ya kuibiana mabwana, ni ujinga tu. Unazungumza ili iweje?”
aliandika mfuasi wa Kajala mtandaoni.KAJALA AFURA
Jitihada za kumpata Kajala aweze kuzungumzia mashambulizi hayo ya Wema hazikuzaa matunda baada ya simu yake kuita bila kupokelewa lakini shosti yake wa karibu alisema Kajala amechukizwa na maneno hayo ya Wema na kamwe hatakuja kukaa naye meza moja, achilia mbali kumzika.
No comments:
Post a Comment